Jumapili , 9th Jul , 2023

Mtoto Yusuph Salum (9) mkazi wa Rutamba Manispaa ya Lindi, ambaye alichomwa moto na mvuke wa maji na mganga wa kienyeji kwa dhamira ya kumtibu ugonjwa wa degedege, amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Lindi Sokoine wakati akipatiwa matibabu ya vidonda hivyo.

Sehemu aliyoungua

Inasemekana kwamba, mama mzazi wa mtoto Yusuph ambaye ni mkazi wa Rutamba, alimpeleka mwanaye nyumbani kwa mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la Jalina Juma Jiwalila, mwenye umri wa takriban miaka 40 kwa lengo la kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa Degedege uliokuwa unamsumbua

Baada ya kumfikisha mganga huyo aliahidi kumtibu na ndipo alipomlaza chali kwenye kitanda ambacho hakikuwa na godoro na kisha chini aliweka nyasi na kuziwasha moto uliopelekea kumuunguza sehemu za mgongoni na kumsababishia majeraha makubwa.

Alisema baada ya tukio hilo mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Lindi kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo umauti umemkuta tarehe 08/07/2023 akiwa bado Hospitalini hapo.

Polisi walipata taarifa hizo na kufika nyumbani kwa mganga huyo ambapo alifikishwa kwenye kituo cha polisi kwa mahijiano zaidi.