Ijumaa , 7th Aug , 2020

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Rombo Joseph Selasini, amevitaka vyama vya upinzani kuhakikisha wanafanya tathmini juu ya wapi walipotoka na wanapoelekea ili ziweze kuwasaidia katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Joseph Selasini

Amesema hayo leo Agosti 7 katika mkutano mkuu wa chama cha NCCR Mageuzi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo wajumbe wanatarajia kupiga kura kwa ajili ya kuwapata wagombea watakao peperusha bendera ndani ya chama hicho.

"Ni vizuri tunavyoingia kwenye mageuzi vyama vyote vya upinzani tufanye tathimini tumetoka wapi tupo wapi, na tunakwenda wapi mbona katika miaka 28 mtoto ameshakuwa mtu mzima anajitegemea na bado tunalilia tu", amesema.

Aidha Selasini amewakumbusha vijana kuwa agenda ya katiba imeanza muda mrefu tangu  tarehe 11/06/1991 ambapo wanamageuzi walikaa katika ukumbi nakudai mageuzi na ndipo chombo cha NCCR kilipoundwa kwa ajili kutafuta marekibisho ya kikatiba.

“Vijana niwakumbushe tarehe 11/06/1991 wanamageuzi tulikutana katika ukumbi huu tukiidai serikali mageuzi baada ya mkutano ule vilizaliwa vyombo viwili cha kwanza NCCR maana yake Baraza la kitaifa kwa ajili ya kutafuta marekibisho ya Katiba, sasa ambao wanasema agenda ya katiba ni yao wanakosea imeanza siku nyingi”.