
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi mwanamke huyo alinyogwa kwa kutumia nguo wakati wakiwa chumbani na mume wake huku sababu ikitajwa mume huyo kuwa na tabia ya ulevi wa kupita kiasi.
Uchunguzi wa awali wa juu ya tukio hilo umeonesha kuwa mama huyo aliuawa siku tatu zilizopita baada ya tathmini ya Jeshi la Polisi kudai mwili wa marehemu huyo ulikuwa umevimba.
Kupitia Kamanda wa Polisi mkoani Manyara, Agustino Senga amesema jeshi hilo linamtafuta mwanaume aliyehusika na tukio hilo na kueleza kuwa endapo litafanikiwa kumpata kupitia wasamalia wema na vyombo vyake vya uchunguzi basi atapelekwa kwenye vyombo vya sharia kujibu mashtaka yake.
“Kwa uchunguzi wetu wa awali, chanzo cha mauaji ni ulevi na tunajua amekimbilia Arusha, lakini niwaahidi kupitia Jeshi la Polisi tutahakikisha tunampata mwanaume huyu ili aweze kujibu tuhuma zake.” Amesema Kamanda Agustino Senga