Anayedai kugeuzwa msukule miezi 4, azungumza

Jumanne , 4th Mei , 2021

Jeshi la polisi wilayani Magu mkoani Mwanza limemuokoa kwenye mikono ya wananchi wenye hasira kali Salome James, mkazi wa Kijiji cha Sato anayedaiwa kuwafanya misukule baadhi ya wakazi wa kijiji hicho na kuwatumikisha kwenye mashamba yake.

Shija Peter, mwananchi anayedai kuchukuliwa msukule

Akizungumza mbele ya wakazi wa kijiji hicho, mmoja wa vijana waliopotezwa na kufanywa msukule, anayeulikana kwa la Shija Peter, amedai kuwa aligeuzwa msukule kwa muda wa miezi minne na mama huyo na kusema kuwa alikuwa analazwa sehemu moja na fisi na kunyweshwa uji huku familia yake ikiwa haijui mahali alipo.

"Nilikuwa na suruali nyeupe na shati nikanyang'anywa nikabaki na bukta, asubuhi tulikuwa tunachukuliwa tunapelekwa shambani kulima, tulikuwa tunalima mchana na usiku lakini kula hakuna tunakorogewa na uji na usiku tunatembezwa kwenye majumba ya watu kutafuta chakula na tulikuwa tunapakwa madawa", ameeleza Shija

Kwa upande wake Seko Nyabanya, ambaye ni mganga wa jadi aliyefanikiwa kumtoa katika hali ya msukule kijana Shija Peter, ameeleza hali aliyokuwa nayo kijana huyo kabla na baada ya kumrudisha katika hali yake ya kawaida na kuweza kujitambua.