"Anayetaka kuwashtaki, anishtaki mimi" - Makonda

Alhamisi , 11th Jul , 2019

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameanza maandalizi kuelekea mkutano mkuu wa nchi za SADC, unaotarajia kufanyika Agosti 2019 jijini Dar es salaam, ambapo leo amekutana na waendeshaji wa mitandao ya kijamii na kuwakabidhi maswali 12,

kwa ajili ya kuwauliza wananchi kuelekea mkutano huo.

Makonda amefikia maamuzi hayo leo jijini Dar es salaam, ambapo ameeleza lengo la mkakati huo, ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na uelewa kuhusiana na mkutano wa SADC, pamoja na kujua kiundani juu ya umuhimu wa mkutano huo kwenye masuala ya biashara.

Makonda amesema kuwa "tufanye jambo litakalotikisa Mkoa wetu, nataka tufanye mashindano yatakayokuwa na zawadi, zawadi ya kwanza itakuwa wewe na kamera yako, na zawadi ya pili itaenda kwa mwananchi utakayefanya naye kazi."

"Nataka siku ya kutoa zawadi iwe tarehe 5 Agosti 2019, nataka kwa yeyote mwenye Platform, asaidie kupatikana kwa majibu ya maswali 12, na mwisho wa siku atajichukulia milioni 3." ameongeza Makonda

Aidha Makonda kuhusiana na ugumu wa kufanya kazi hiyo amesema kuwa "SADC kuna kila kitu,pia hii ni kazi ya Serikali hakuna wa kukuhoji,muifanye kwa moyo mkunjufu bila hofu, kama mtu atakushtaki aanze kunshtaki mimi. "