Jumatatu , 5th Mei , 2025

Msanii Marioo amefunguka sababu za kukosekana kwenye harusi ya msaniii juma jux licha ya kuwa wawili hao ni marafiki,mbali na hilo pia Bad ameweka wazi kuwa hana ugomvi wowote ule na Jux

Pichani ni Marioo na Jux

 

"Jux ni kaka yangu ni moja kati ya mama zangu wakubwa kabisa,nikiambiwa nitaje kaka zangu ninaowapenda na naamini wana upendo wa kweli na mimi nitamtaja namba moja'' Amesema marioo

"#Jux kanizidi umri mrefu sana kanizidi uzoefu kwenye kazi kwahiyo ni ngumu sana mimi na yeye kugombana,zinawezakuwa ni story tu kwasababu watu hawajaniona kwenye harusi yake (Nigeria) lakini ni mtu ambaye nafurahi mafanikio yake na yeye anafurahia mafanikio yangu" Amesema marioo

"Siku ya ndoa yake mimi nilikuwa nimepokea hela ya kazi,nilienda kuimba kwenye Birthday ya mtoto wa Lugumi kwahiyo nilikuwa nishachukua hela nisingeweza kuomba niende kule (Nigeria) lakini kwasababu shughuli ziko mbili nimeweza kubalance hii inayokuja nisikose''   Amesema marioo