Jumatano , 25th Aug , 2021

Jeshi la Polisi Tanzania, limethibitisha kuuawa kwa watu wanne wakiwemo Askari watatu kwenye mapambano ya kurushiana risasi yaliyotokea leo eneo la Daraja la Selander jirani na Ubalozi wa Ufaransa, Dar es Salaam, likihusisha mtu mmoja mwenye silaha ambaye naye ameuawa kwa risasi.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas

Taarifa ya vifo hivyo imetolewa leo Agosti 25, 2021, na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas, alipofika eneo la tukio.

Aidha, kufuatia tukio hilo Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa pole kwa familia za Askari wanne akiwemo yule wa kampuni ya ulinzi ya SGA waliofariki baada ya mtu aliyekuwa na silaha kuwashambulia katika eneo la Selander, karibu na Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam, na ameagiza polisi kuchunguza kwa kina na kusema mtu huyo amedhibitiwa na hali ni shwari.