Jumatano , 11th Mar , 2020

Msanii wa Injili Bella Kombo, amefunguka na kusema yupo tayari kumsamehe mwanaume wake hata kama akimsaliti kwa sababu ataangalia haki iko wapi.

Msanii wa injili Bella Kombo

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Bella Kombo amesema yeye ni mlokole halisi, ambaye ameokoka na Mungu amemuita na kumchagua ili kumtumikia katika maisha yake yote yaliyobaki kwa sababu huko nyuma alikuwa mkosefu sana.

"Najivunia kuwa mwanamke, najiona mwenye nguvu na ninaweza kuyashinda majaribu makubwa yanapokuja, halafu wanawake tuna moyo wa uvumilivu, mimi naweza kumvumilia  hata  mwanaume wangu akinisaliti kwa sababu nitaangalia upande wa haki ni upi" ameeleza Bella Kombo.

Pia msanii huyo wa Injili ameendelea kusema  "Siwezi kuolewa kwa mara ya pili kwa sababu ndoa unatakiwa uolewa mara moja, lakini Mungu ndiye anayenipangia kama akipanga niolewe tena siwezi kukataa japokuwa sasa hivi nina ndoa tayari" ameongeza.