Athari za Mvua : Paa la Nyumba laangukia nguzo

Ijumaa , 17th Jan , 2020

Wakazi wa Mtaa wa Nsemulwa kwa Mkumbo Kata ya Uwanja wa ndege Mkoa wa Katavi wamekumbwa na taharuki kubwa, baada ya kunyesha Mvua iliyoambatana na upepo mkali ulioezua Paa la Nyumba lililoenda kuangukia juu ya nyaya za umeme.

Picha si halisi

Kwa mujibu wa wakazi hao baada ya Paa hilo kudodondokea nyumba pia imesababisha moto mdogo, ulioambatana na Moshi mkali katika nguzo zilizo karibu na nyaya hizo.

Akizungumzia tukio hilo Dotto Chacha ambaye ni Mkuu wa Umeme Mkoa wa Katavi, amesema licha ya nguzo hizo kupata hitilafu iliyosababishwa na paa la nyumba baada ya kuangukia nyaya hizo ila hakuna madhara yaliyotokea.

Tazama video kamili hapo chini.