Katika siku ya mwisho ya mkutano wa kilele mjini Addis Ababa, Umoja wa Afrika umesema utaendeleza kutozitambua Burkina Faso, Guinea, Mali na Sudan ambazo zote zinatawaliwa na viongozi wa kijeshi kufuatia mapinduzi.
Kamishna wa masuala ya kisiasa, Bankole Adeoye, alisema AU iko tayari kuzisaidia nchi hizo kurejea katika utaratibu wa kikatiba na kusaidia demokrasia kuota mizizi.
Viongozi katika mkutano huo pia walikubaliana kuendelea na mipango ya makubaliano ya biashara huru ikiwa ni pamoja na karibu kila nchi barani Afrika.






