Alhamisi , 21st Nov , 2019

Msanii wa Bongo Fleva na Diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini, Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mhe. Clayton Revocatus Chipando maarufu Baba Levo, leo Novemba 21, 2019, ameshinda Rufaa yake katika Mahakama kuu Mkoa wa Kigoma.

Baba levo katikati (mwenye shati nyeupe) akiwa na ndugu zake baada ya kutoka mahakamani.

Awali alihukumiwa kifungo cha miezi 6 katika mahakama ya Mwanzo Mwandiga, alipokata rufaa katika mahakama ya Mkoa, akahukumiwa kifungo cha Mwaka 1 na siku 2 jela, ambapo ameshinda katika Rufaa yake mahakama kuu.

Baba levo alihukumiwa kwa kosa la kumshambulia Askari wa Usalama Barabarani.

Katika huku ya leo, Jaji amefuta hukumu ya mahakama ya wilaya na Baba levo yupo huru kutokana kifungo chake kilikuwa kinaishia tarehe 11/11/2019 siku ya Jumanne.

Baada ya hukumu, Diwani wa Kata ya Kigoma Hussein Kaliyango, amesema 'tunashukuru maamuzi ya mahakama kuu haki imetendeka na sio haki kutendeka tu haki imeonekana imetendeka'.