Jumatatu , 29th Aug , 2022

Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Sunday (46), mkazi wa mtaa wa Mkudi, Kata ya Nyamanoro Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza, anadaiwa kumbaka mtoto wa 8 (Pichani) na kumsababishia maumivu makali ikiwemo kumuharibu kisaikolojia.

Mtoto aliyebakwa

Mtoto huyo akizungumzia tukio hilo amesema mwanaume huyo alimuita wakati akiwa anacheza na kumvutia ndani.

"Nilikuwa nacheza ndipo Sunday akaniita akanivuta ndani akaniambia naomba nikubake nikakataa, nilivyokataa nikataka kupiga kelele akaniziba mdomo akanitishia kisu, akanivua nguo akanibaka kisha akanipa shilingi mia tano akamaliza akafunga mlango akaondoka baada ya mama kujua nimebakwa akamuita bibi ndipo tukaenda polisi" ameeleza mtoto huyo

Wakizungumza kwa uchungu wazazi wa mtoto huyo wameviomba vyombo vya dola kuwasaidia kutokana na mtoto wao kuharibiwa na kuambulia kupata maumivu makali huku akitakiwa kutumia dawa mwezi mzima ili kumuepusha na maambukizi ya virusi vya ukimwi lakini wanashangaa mtuhumiwa akiwa nje kwa dhamana licha ya kumfungulia kesi ya ubakaji na Ushahidi kuwepo.