Alhamisi , 6th Mei , 2021

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewajulisha Waislamu na Wananchi wote kwa ujumla kuwa Sikukuu ya Eid El-Fitr itakuwa Alhamisi Mae 13, 2021 au Ijumaa Mei 14, 2021.

PIcha ya ishara ya mwezi kuandama

Taarifa ya BAKWATA imefafanua sababu ya tarehe hizo mbili ni kutegemeana na kuandama kwa mwezi.

Sherehe za Eid El- fitr kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika Mkoa wa Dar es salaam ambapo swala ya Eid itaswaliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 1:30 asubuhi.