Jumanne , 8th Sep , 2015

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka tume ya uchaguzi kuchukua hatua kwa viongozi wanaokiuka sheria za uchaguzi ikiwemo kufanya kampeni kwenye nyumba za ibada au kuwatumia viongozi wa dini kwenye kampeni kwa ajili Ya kuomba kura kwa wananchi

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nauye

Akiongea na waandishi wa habari katibu wa uwenezi wa chama hicho Nape Nnauye amesema kuwa ni vizuri kwa watanzania kuwa makini kwa wakati huu wa kampeni na kuhakikisha hawashawishiki kuiharibu amani ya nchi kwa kufuata kauli zinazotolewa na wanaowania nafasi za uongozi kwa manufaa yao binafsi.

Bw, Nnauye amesema kuwa Mgombea Urais wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa alikiuka kifungu cha sheria ya taifa ya uchaguzi sura 343 ambayo hairuhusu kufanya kampeni sehemu za ibada wala kuwatumia viongozi wa dini kupiga kampeni.

Aidha Nape Ameitaka Tume ya Uchaguzi NEC ni kuchumkulia hatua za kisheria mh. Lowasa kwa kukiuka Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015, wakati huo huo Nnape ameitaka pi jamii nzima kupiga vita vitendo vyote vya kibaguzi kwa misingi ya Udini, Ukanda, Ukabila, Jinsi n.k

Hatua hiyo imekuja baada ya Jumapili iliyopita katika Kanisa la KKKT Mjini Tabora Mh. Edward Lowasa kuomba waumini wa kanisa hilo wamuombee dua ili ashinde urais.