Jumapili , 17th Feb , 2019

Baada ya Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume kukosa nafasi ya kuhutubia katika siku ya sheria Februari 06, 2019, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za binaadamu, Bi Helen Kijo-Bisimba amesema anaamini kwamba waandaji waliogopa kusikia vitu was

Mkurugenzi Mtendaji Mstaafu wa Kituo cha Sheria na Haki za binaadamu, Bi Helen Kijo-Bisimba

Bi. Kijo-Bisimba ameyasema hayo wakati akizungumza na www.eatv.tv katika kipindi maalumu ambapo ameongeza kwamba sababu ya ufinyu wa muda iliyotolewa haina uzito mbele ya mdau wa sheria kama TLS.

"Mimi nakataa hakuna ufinyu wa muda kwa kuwa muda unapangwa. TLS ni mdau mkubwa wa mahakama. Kama ni ufinyu wangeondolewa watu wote na kuwaacha TLS. Kwa maoni yangu naona kabisa hawakutaka au walihofu kusikia kitui ambacho wao hawapendi kusikia", amesema Bi Kijo-Bisimba

Siku moja kabla maadhimisho ya wiki ya Sheria, Rais wa Chama hicho Bi Karume alitoa taarifa kwamba, "leo nimepokea barua inayosema mimi, TLS na Mwanasheria mkuu wa Serikali, hatutoweza kuhutubia Umma kutokana na ufinyu wa muda. Haijawahitokea kwa muda wa zaidi ya miaka 20 kwenye historia ya kuwepo kwa TLS kushindwa kuhutubia kutokana na ufinyu wa muda".