Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
Hayo ameyabainisha hii leo Oktoba 28, 2022, na kusema Tanzania bado inakabiliwa na upungufu wa madaktari bobezi na madaktari bingwa wa magonjwa ya binadamu hali inayosababisha serikali kupeleka baadhi ya wagonjwa nje ya nchi kupatiwa matibabu kwakua hayapatikani katika hospitali za ndani ya nchi.
Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema bado kuna ongezeko la wagonjwa wa afya ya akili na wagonjwa wa mifupa kutokana na ongezeko la ajali za barabarani.