
Miguu ya mtoto
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Safia Jongo, wakati anatoa taarifa kwa waandishi wa habari ambapo amesema taarifa za tukio hilo walizipata kwa wasamaria wema ambao walimuona binti huyo akiwa mjamzito lakini ghafla wakashangaa kumuona hana mtoto wala ujauzito ndipo wakatoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.
"Tulivyopata taarifa hiyo Jeshi la Polisi lilimchukua huyo binti na kufanya nae mahojiano ambapo alikiri kwamba ni kweli alijifungua mtoto ambae alikuwa na umri wa wiki mbili lakini kutokana na kwamba yeye kazi yake ni ya kuuza bar lakini pia anajiuza mwili wake, kwahiyo yule mtoto akawa ni kero kwake anashindwa kwenda kufanya biashara yake hivyo akaamua kuchimba shimo na kumfukia huyo mtoto", amesema RPC Jongo.
Kamanda Jongo ameendelea kuwaomba wananchi kutoa taarifa pale wanapokuwa na mashaka na mtu kufanya vitendo vya kikatili ili kupunguza vitendo hivyo na kupata jamii iliyo salama.
"Ni kitendo Kibaya, kitendo cha kikatili sana na mbaya zaidi kilitokea kipindi cha siku 16 za kupinga ukatili, kwahiyo huo ni moja ya ukatili ambao unatokea, kwahiyo niisihi jamii pale wanapowaona mabinti na maisha ambayo hayampendezi Mungu na maisha ambayo hayapendezi jamii na maisha ambayo yapo kinyume na sheria na kanuni za nchi yetu ni vema kutoa taarifa," ameongeza Kamanda Jongo