Ijumaa , 2nd Jan , 2026

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Ju Ae amekuwa akionekana mara kwa mara na kwa umaarufu mkubwa zaidi kwenye vyombo vya habari vya serikali, jambo ambalo limechochea nadharia kutoka kwa wachambuzi kwamba huenda akawa kiongozi wa kizazi cha nne wa nchi hiyo.

Binti wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, Ju Ae ambaye anachukuliwa na wengi kuwa anaandaliwa kuwa mrithi wa kiongozi huyo, ameandamana na wazazi wake katika ziara yake ya kwanza ya hadharani kwenye makaburi ya Kumsusan ili kutoa heshima kwa viongozi wa zamani wa taifa hilo, kulingana na picha zilizochapishwa na vyombo vya habari vya serikali leo Ijumaa.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Ju Ae amekuwa akionekana mara kwa mara na kwa umaarufu mkubwa zaidi kwenye vyombo vya habari vya serikali, jambo ambalo limechochea nadharia kutoka kwa wachambuzi na shirika la kijasusi la Korea Kusini kwamba huenda akawa kiongozi wa kizazi cha nne wa nchi hiyo.

Wachambuzi wametafsiri kuonekana kwa mara ya kwanza kwa Ju Ae katika jumba la Kumsusan kama hatua ya kimkakati ya baba yake kuelekea Mkutano Mkuu ujao wa chama tawala, ambapo urithi wake wa uongozi unaweza kurasimishwa.

Katika ziara hiyo ya Januari 1, Kim Jong Un pia aliandamana na mke wake, Ri Sol Ju, pamoja na maafisa wakuu wa serikali. Picha za shirika la habari la serikali KCNA zilimuonyesha Ju Ae akiwa amesimama kati ya wazazi wake katika ukumbi mkuu wa Ikulu ya Jua ya Kumsusan.

Kim Ju Ae, anayeaminika kuzaliwa mwanzoni mwa miaka ya 2010, alihudhuria maadhimisho ya Mwaka Mpya mwaka huu. Mnamo Septemba 2025, alisafiri kwenda Beijing na baba yake katika safari yake ya kwanza ya hadharani nje ya nchi. Korea Kaskazini haijawahi kuthibitisha rasmi umri wa Ju Ae.

Kim Jong Un hutembelea makaburi ya Kumsusan kuwaenzi babu yake na mwanzilishi wa taifa, Kim Il Sung, pamoja na baba yake Kim Jong Il, katika tarehe na maadhimisho muhimu, kama ishara ya kuthibitisha urithi wa kifalme wa nchi hiyo yenye silaha za nyuklia.