Jumatano , 18th Sep , 2019

Mbunge wa Segerea Bonnah Kamoli, amesema huenda akagombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo amedai anadhani yeye anafaa kurithi kiti cha Rais wa sasa Dkt. John Pombe Magufuli, ifikapo 2025.

Akizungumza katika kipindi cha Kikaangoni kinachorushwa kwenye ukurasa wa Facebook na Youtube ya East Africa TV, ambapo amesema kwenye uchaguzi huo huenda akafaa hivyo kama atapewa dhamana na chama chake.

"Sijafikiria kugombea Urais kwasasa ila ikifika 2025 huenda nikagombea maana nitakuwa na uzoefu tayari, nadhani nitafaa kumrithi Rais Magufuli" amesema Mbunge Bonnah Kamoli

Kuhusiana na suala kutoa rushwa ya ngono ili apate Ubunge, Mbunge Kamoli amesema hajawahi kutoa rushwa ya ngono, ili apate nafasi hiyo bali yeye ndiyo alikuwa Mbunge asiyekuwa na kipato katika orodha ya Wabunge.

"Sijawahi kutoa rushwa ya ngono katika harakati zangu za kisiasa, sijatumia pesa yoyote kuwa Mbunge, badala yake mimi ndiyo sikuwa na kitu chochote kati ya wagombea wote ndani ya CCM katika Jimbo la Segerea" amesema Mbunge Bonnah Kamoli

Fuatilia mahojiano kamili hapo chini.