
Waziri wa habari wa Somalia amesema kwamba bwana Nadir alikua ni mkuu wa propaganda za al Shabab
Taarifa ya waziri huyo imeongeza kwamba al-Shabab ilikua ikimtegemea Nadir kama mrithi wa kiongozi wa sasa wa kundi hilo hatari. aitwae Ahmed Omar Diriye, maarufu kwa jina la Abu Ubaidah, ambaye taarifa zinasema kwamba ana hali mbaya ya afya.
Vyombo vya habari vinasema kwamba Nadir alipoteza maisha katika shambulizi la anga. Kwa mujibu wa waziri huyo mashambulizi hayo yalifanywa na vikosi vya usalama nchini Somalia kwa msaada wa majeshi washirika.