
Mbunge wa Viti Maalum Ester Bulaya
Kauli za wabunge hao zimekuja baada ya mwenyekiti wa bunge Najma Murtaza Giga kutoa tangazo kwa wabunge wote kuwa bunge limeanza mchakato wakutafuta nafasi kwa wabunge vijana kwenda kupata mafunzo hayo ya kijeshi kama ilivyiowahi kufanyika siku za nyuma
Bulaya akiomba muongozo kuhusu tangazo hilo amesema kwanini sasa utaratibu usibadilike kutoka kuwa hiari na kuwa ni lazima kwa wabunge wote vijana kwenda kupata mafunzo ya JKT ili kuisaidia nchi kuwa na askari wengi wa ziada
Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Musukuma akiomba muongozo kuhusu tangazo hilo amesema ni wakati sasa wa wabunge wote kwenda kupata mafunzo hayo bila kujali wazee au vijana ili kuwajengea ukakamavu na uzalendo
Mwenyekiti wa Bunge Najma Murtaza Giga amesema kwa kuwa hilo ni tangazo limetolewa na bunge atapeleka maoni ya wabunge hao kwa wahusika