Alhamisi , 8th Mei , 2014

Majadiliano ya hotuba ya Makadirio ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu yanaendelea tena leo mjini Dodoma ambapo hakuta kuwa na kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda kama ilivyo desturi.

Waziri mkuu wa Tanzania, Mizengo Kayanza Peter Pinda.

Akihairisha jana usiku majadiliano hayo ya ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Spika wa Bunge Anne Makinda amesema kwa kuwa majadiliano hayo yanaendena na maswali kwa waziri mkuu, wabunge watatumia fursa hiyo kuendelea kumuuliza maswali waziri mkuu wakati wakijadili.

Aidha, Spika Makinda amewataka wabunge kuwa na uvumilivu na kuepuka kutumia lugha kali kwani kitendo hicho huchochea upande wa pili nao kujibu kauli hizo na kupelekea kuondoa hali ya utulivu bungeni.