Alhamisi , 31st Jul , 2025

Wakati Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas ameelezea uamuzi huo kuwa wa kihistoria na ujasiri na utaimarisha amani, utulivu na usalama katika eneo hilo, Israeli imelaani mara moja.

Canada imejiunga na Ufaransa na Uingereza, washirika wengine wa nchi zenye uchumi mkubwa duniani, maarufu kama G7, kutangaza nia yake ya kutambua taifa huru la Palestina katika Mkutano Mkuu ujao wa Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka huu.

Kauli hii ya Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney aliyoitoa jana Jumatano, Julai 30 mbele ya waandishi wa habari, imeikasirisha Israeli, ambayo inaona kuwa ni sehemu ya kampeni potofu ya shinikizo la kimataifa.

Carney amesisitiza kuwa kiwango cha mateso ya binadamu huko Gaza hakivumiliki na hali inazidi kuzorota kwa kasi, pia ameeleza kuwa anaamini mabadiliko haya ya sera ni muhimu ili kuhifadhi matumaini ya suluhu la serikali mbili.

Wakati Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas ameelezea uamuzi huo kuwa wa kihistoria na ujasiri na utaimarisha amani, utulivu na usalama katika eneo hilo, Israeli imelaani mara moja.

Katika taarifa yake, Ubalozi wa Israeli nchini Canada umeuchukulia kama sehemu ya kampeni potofu ya shinikizo la kimataifa ambayo inafanya msimamo wa Hamas kuwa mgumu katika meza ya mazungumzo katika wakati mgumu.