Ijumaa , 18th Sep , 2015

Chama cha Mapinduzi CCM, mkoa wa Iringa kimewaagiza makada wake na wanachama wa chama hicho kujiepusha na siasa zenye mlengo wa kupandikiza chuki miongoni mwa jamii ili kuepuka uvunjifu wa amani uchaguzi mkuu.

Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga

Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga ametoa wito huo wakati akihutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni za udiwani jimbo la Iringa mjini ambapo amesema watanzania ni wamoja kwa hiyo itikadi za kisiasa zisiwagawe na kuvuruga amani ya nchi.

Kauli ya Mtenga imekuja siku moja baada ya kuripotiwa kwa vurugu kati ya wafuasi wa CHADEMA, na CCM, ambapo mmoja wao alijeruhiwa na kutibiwa hospitalini.

Akinadi sera za chama hicho, mgombea udiwani wa kata ya Kihesa Kanani Kihongosi ameahidi kusimamia kikamilifu ilani ya chama hicho ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa kata hiyo.