Jumatatu , 28th Sep , 2015

Mgombea nafasi ya ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Fredrick Mwakalebela ameahidi kuanzisha VOCOBA na kutoa mikopo kwa akina mama ili kuinua uchumi wao.

Mgombea nafasi ya ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Fredrick Mwakalebela.

Bw. Mwakalebela ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Kwakilosa manispaa ya Iringa amesema ikiwa atachaguliwa ataboresha huduma za jamii.

Naye mgombea wa nafasi ya udiwani kupitia chama cha CCM kata ya Kwakilosa Bw. Amidi Mbata amesema ikiwa atachaguliwa ataboresha huduma za afya.

Hata hivyo, Bw. Mbata ameahidi kushirikiana na wananchi wa kata ya Kwakilosa katika kufanya masuala ya kijamii ili kuleta maendeleo.