
Heche amesema hayo ikiwa ni siku moja baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa huo, Frank Kamugisha kumtaka Askofu Kakobe aende kufanya toba na kisha kuwaomba radhi wana CCM wa Dar es salaam kwa kuacha miiko ya kidini na kushindwa kutumia busara na kisha kusema hovyo.
Akizungumza jana na Wanahabari Kamugisha alivitaka vyombo vinavyohusika na sheria vihakikishe hakuna mtu anayepata fursa ya kumtukana au kumbeza Rais wa nchi na kufafanua kwamba Rais amejipambanua katika kuwasaidia wananchi na anafanya mambo hayo kwa udhati wa moyo wake hivyo mtu anyebeza moja kwa moja atakuwa msaliti.
Heche amandika kwenye ukurasa wake wa Twitter na kusema kwamba "CCM kama mnataka kujibu hoja za Askofu Kakobe kwa niaba ya Rais Magufuli na Serikali jibuni kwa hoja, sio kuropoka! kazi za wachungaji ni kukemea maovu yote yaliyopo duniani, watu wanapotea, wanapigwa risasi, wanaokotwa baharini, sheria za nchi hazifuatwi, haya yatakemewa na kila mtanzania" Heche.