Jumatano , 16th Jul , 2025

Msanii wa muziki wa Afrobeats, Ayra Starr, amejiunga rasmi na kampuni ya kimataifa ya burudani Roc Nation, inayomilikiwa na rapa Jay-Z.Taarifa hii imethibitishwa baada ya jina la Ayra kuwekwa kwenye tovuti rasmi ya Roc Nation.

Ayra Starr, ambaye bado yupo chini ya lebo ya Mavin Records inayoongozwa na Don Jazzy, ataendelea kusimamia kurekodi na usambazaji wa muziki wake kupitia Universal Music Group. Kwa upande mwingine, Roc Nation itakuwa na jukumu la kusimamia:Matamasha na maonyesho ya kimataifa, Mikataba ya matangazo na biashara,Uhusiano wa kimataifa na vyombo vya habari,Ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya burudani.

 

Kujiunga kwa Ayra Starr na Roc Nation ni hatua muhimu sio tu kwa msanii mwenyewe, bali pia kwa muziki wa Afrobeats unaoendelea kushika kasi duniani. Ushirikiano huu unatarajiwa kufungua milango zaidi kwa Ayra katika soko la kimataifa, na pia kuimarisha nafasi ya wasanii wa Kiafrika kwenye majukwaa ya dunia.

 

Ayra Starr alijitokeza kwa mara ya kwanza mwaka 2021 kupitia wimbo wake maarufu "Away", na tangu wakati huo amekuwa na mafanikio makubwa kwa nyimbo kama "Rush", "Bloody Samaritan", na "Sability".