Jumanne , 2nd Sep , 2014

Pamoja na kuwepo kwa malalamiko ya kufumuliwa kwa rasimu ya maoni ya katiba, baadhi ya wadau wamesema kuna umuhimu wa kuwepo kwa maoni mapya ambayo yana umuhimu na hayakuwepo kabisa kwenye rasimu hiyo.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Taifa kupitia chama cha Mapinduzi - UVCCM, Sixtus Mapunda.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Taifa kupitia chama cha Mapinduzi UVCCM jijini Mbeya Sixtus Mapunda amesema hayo wakati wa sherehe za kumwapisha Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Rugwe Richard Kasesela.

Mapunda amesema kuwa Rasimu ya sasa kuna vitu vingi havijawekwa ambavyo vina mslahi kwa wananchi ambapo ametaja baadhi ya vipengele ambavyo vimeongezwa ili kuboresha rasimu hiyo.

Wakati huo huo, wakazi zaidi ya elfu 3 wakata ya daraja mbili Jijini Arusha nchini Tanzania ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikosa huduma za afya na kulazima kutembea umbali mrefu ,wameaanza kupata huduma hiyo kufuatia kakamilika kwa ujenzi wa kituo cha afya cha kata hiyo.

Wakiongea na kituo hicho baadhi ya wakazi wa kata hiyo wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilazimika kutembea zaidi ya kilometa kumi na nne kufuata huduma hiyo jambo ambalo limekuwa likihatarisha maisha yao hususani wanawake

Mganga wa kituo hicho Dkt David Mganya akisoma risala katika uzinduzi wa kituo hicho kilichozindulia na kiongozi wa mbio za Mwenge amesema kukamilika kwa kituo hicho kutasaidia katika kufikia malengo ya millennia ya kupunguza vifo wa wakina wajawazito na watoto wachanga.