Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

CHADEMA yaipigia goti NEC

Alhamisi , 12th Jul , 2018

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia Katibu Mkuu wake Dkt. Vicent Mashinji wameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusimamia haki katika uchaguzi mdogo wa Ubunge na udiwani ambao umepangwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu kwa kata 77 za Tanzania Bara.

Katibu Mkuu wake Dkt. Vicent Mashinji

Dkt. Mashinji ametoa Kauli hiyo leo Julai 12, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kuitaka Tume hiyo kuendesha uchaguzi uliokuwa huru ili mradi amani na utulivu iendelee kuwepo nchini.

"Katika uchaguzi huu wa marudio kumeanza kujitokeza vitendo vya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi, ikiwemo kughushi saini za viongozi ili kuhalalisha wagombea katika Halmashauri ya Tunduma mkoani Songwe kupitishwa kinyume na sheria. Tunaviomba vyombo vya dola kuwachukulia hatua wote waliohusika. Kutokuwa na uchaguzi huru kunaweza kusababisha machafuko katika nchi", amesema Dkt. Mashinji.

Pamoja na hayo, Dkt. Mashinji ameendelea kwa kusema "tunahitaji kuwepo na Tume huru ya uchaguzi na katika uchaguzi huu, Tume isimamie haki na hizi figisu figisu zilizoanza kujitokeza izimalize mapema pamoja na matukio ya wagombea kukamatwa na kunyang'anywa fomu zao za ushiriki".

Uchaguzi huo mdogo wa marudio umekuja baada ya kuwepo wazi Jimbo la Buyungu Mkoani Kigoma kufuatia Mbunge Kasuku Bilago kufariki dunia mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu pamoja na madiwani wa maeneo mbalimbali kuyaacha majimbo yao na kujiunga CCM kwa lengo la kumuunga mkono Rais Magufuli.

HABARI ZAIDI

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao