Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

CHADEMA yamkana Mbunge wake

Alhamisi , 11th Oct , 2018

Baada ya Mbunge wa Jimbo la Ukerewe mkoani Mwanza kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Michael Mkundi kutangaza  kujiuzulu na kuomba kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) usiku wa jana Oktoba 10, CHADEMA wamekanusha tuhuma alizozitoa dhidi ya chama hicho.

Pichani, aliyekuwa Mbunge wa Ukerewe (CHADEMA), Joseph Mkundi na Mkurugenzi wa mawasiliano CHADEMA John Mrema.

Kupitia barua aliyomwandikia Spika wa Bunge Job Ndugai, Mkundi amesema kuwa amechukua uamuzi huo baadaya kutopatiwa ushirikiano na chama chake katika maafa ya kuzama kwa kivuko cha Mv. Nyerere kilichopelekea vifo vya watu zaidi ya 230.

Akizungumza na www.eatv.tv Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema kuwa Mbunge huyo alipatiwa ushirikiano ikiwemo wabunge kuchanga michango na kufika kisiwani Ukara.

"Wabunge walitoa rambirambi zao pamoja na kufika kwenye eneo la tukio pamoja na baadhi ya viongozi labda yeye aseme kama alitaka nani na nani wafike huenda kuna watu alitaka wafike na hawakufanya hivyo", amesema Mrema.

Mrema ameongeza kuwa chama kimeshangazwa na tuhuma hizo na wamejaribu kumtafuta lakini hakupokea simu na baadae hakupatikana tena, na kusema kuwa wanamtakia kila la heri katika maisha yake mapya anayokwenda kuanza huko aendako.

Katika barua yake kwa Spika wa bunge ya kujiuzulu uwanachama wa chama chake cha zamani (CHADEMA) na kujiuzulu nafasi yake ya Udiwani na Ubunge, medai kuwa Chama chake cha zamani (CHADEMA) kimepoteza heshima na utu baada ya kumtelekeza katika kipindi ambacho alihitaji msaada na ushirikiano kutoka kwenye chama hicho na uongozi wake katika kipindi cha msiba wa ajali ya Kivuko cha MV Nyerere, iliyotokea Septemba 20, 2018.

Joseph Mkundi anakuwa Mbunge wa tano kutoka CHADEMA kuhama na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi kwa kile wanachodai kuwaletea wananchi maendeleo akiungana na Mwita Waitara, Julius Kalanga, Chacha Marwa Ryoba na Godwin Moleli.

HABARI ZAIDI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu

Mwili wa Boaz Sanga, Mwanafunzi wa CHuo cha SAUTI Mwanza baada ya kupatikana Pembezoni wa Ziwa Viktoria

Mwanafunzi wa SAUTI afariki akijaribu kuogelea

Luteni Jenerali Charles Muriu Kahariri, CDF Mpya wa Kenya

Luteni Charles Muriu ateuliwa kuwa CDF mpya Kenya

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa 124%

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita