
Wanachama wa CHADEMA
Akizungumza na wandishi wa habari jijini humo, Mwaitege amesema kuwa amefikia uamuzi huo ili kuokoa maisha yake kutokana na vitisho alivyokuwa anavipata kutoka kwa wanachama wenzake wa chama hicho ambao walikuwa wanamtishia maisha.
Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbeya Mjini, Agustino Mwadalu amesema chama hicho kiko tayari kumpokea mwanachama yeyote wa upinzani ambaye ni msafi na anataka kuhamia katika chama hicho kwa ajili ya maendeleo.
"Ninamkaribisha ndugu yangu Katibu wa Chama wa CHADEMA, awe huru, aje kwenye chama ambacho kina sera, chama ambacho kina upendo na kwenye chama ambacho kimechukua dhamana ya kuwaongoza Watanzania, chama kinachoishi na Watanzania na kinachoongoza kwa m,ujibu wa sheria", amesema Katibu huyo wa CCM.
Kabla ya Mwaitege kutangaza uamuzi huo, Mwezi Julai mwaka jana Chadema kilipoteza madiwani wanne ambao walihamia CCM akiwemo aliyewahi kuwa Naibu Meya wa kwanza kupitia chama hicho, David Ngogo.