Vitafunwa
Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 20, 2022, Bungeni jijini Dodoma, wakati akitoa kauli ya serikali kuhusu malalamiko ya watanzania kuhusu tozo za miamala ya kielektroniki
"Ni dhahiri kwamba punguzo hili (Tozo kufutwa) litapunguza mapato ya serikali ninaelekeza fedha hizi zifidiwe kutoka kwenye kubana matumizi mengineyo ndani ya serikali ambayo hayataathiri utekelezaji wa majukumu ya msingi ya mafungu husika," amesema Waziri Nchemba
Aidha Waziri Nchemba akaongeza, "Tutafute maeneo tukate kwenye chai , vitafunwa, misafara kwenye safari za ndani na nje kweny wizara zetu, tukate mafunzo ya semina, matamasha, warsha makundi yanayokwenda kugkagua miradi ile ile yanakwenda makundi tofauti taofauti ,".