Jumatatu , 5th Sep , 2016

Washirika wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wamemtaka kiongozi huyo kubadilisha mwelekeo wa sera zake za wakimbizi baada ya chama chake cha CDU kushindwa katika uchaguzi wa kimkoa

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel

Wakati CDU kikifanya vibaya, chama ninachopinga sera za uhamiaji cha AfD kimeshinda uchaguzi huo.

Chama hicho cha mlengo wa kulia AfD kilichoundwa miaka mitatu iliyopita kilijipatia uchindi kwa kuwa chama cha pili katika jimbo hilo la nyumbani kwake Markel jimbo la Mecklenburg-Magharibi mwa Pomerania, kwa kupata asilimia 21.

Kiongozi mwandamizi wa CDU amelaumu wimbi la wakimbizi kuingia nchini humo bila nyaraka kuwa ndicho chanzo cha chama hicho kuanguka

Wakimbizi na wahamiaji zaidi ya milioni 1.1 wameingia nchini Ujerumani katika kipindi cha mwaka 2015 baada ya nchi hiyo kulegeza udhibiti mipakani katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Kiongozi wa AfD huko -MagMecklenburgharibi mwa Pomerania, Leif-Erik Holm, amesema huenda huo ukawa mwanzo wa wa mwisho wake kiutawala Kansela Angela Merkel