Alhamisi , 10th Nov , 2022

Siku moja baada ya jeshi la polisi kuwakamata watu watano wanaohusika na mauaji wa mtu mwenye ualbino, Chama cha watu wenye ualbino mkoa wa Mwanza TAS kimelaani watu wanaoendelea kutekeleza mauaji hayo na kutaka adhabu kali ichukuliwe dhidi yao

Watu wengine kama wana jamii ya kwimba walivyotoa ushirikiano na hao watu wakaweza kukamatwa kwa mauaji hayo ya mwenzetu waendelee kulipa ushirikiano jeshi letunla polisi yunavykatwa viungo vyetu hatufurahi tunayo haki ya kuishi kama mtu mwingine tunaomba tufanye mambo yetu kwa uhuru’

‘Kwahiyo kwakeli kuna sheria ya kunyongwa basi wahusika wanyongwe kwa waliokatisha haki ya kuishi ya mwenzetu na watu wa haki za binadamu tumekuwa tukiwalalamikia sana kuwatetea wanaofanya maovu’

Kutokana na haya mauaji yaalbino tutashindwa kuejesha mikopo ya halmashauri tunaomba wasituue