Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

CHAMAWATA yawasilisha kilio kwa serikali,waajiri

Jumanne , 18th Aug , 2020

Sekta ya usafirishaji nchini imetajwa Kama chachu ya kuchangia kwa Kasi ukuaji wa Uchumi endapo Serikali itazidi kutengeneza mazingira rafiki kusimamia wadau,mifumo ikisimamia Sera.

Kauli hiyo inakuja Mara baada ya uwepo wa malalamiko mbalimbali ya madereva wanaosafirisha mizigo masafa Marefu kuwa Baadhi ya vipengele havifuatwi na waajiri wao ikiwemo mikataba licha ya Serikali kuweka wazi Sheria na utaratibu.

EATV  imefanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa chama cha wafanyakazi wa maroli Tanzania(CHAMAWATA) Greyson Wimile Ambaye ameweka uhalisia ulivyo katika suala la mikataba.

"Ni kweli ndugu mwandishi tunachangamoto ya mikataba na inayotolewa mingi haikidhi masharti ya Ile iliyotolewa na serikali lakini waajiri bado wamekuwa sio waaminifu katika hilo."

Amesema huko nyuma serikali tayari iliweka utaratibu wa mikataba akiiomba wizara ya kazi kupitia maafisa wake kupita katika Makampuni yote kuona Kama yanafuata miongozo iliyowekwa.

Sera ya usafirishaji bado sio rafiki unajua uchumi unabebwa kwa kikubwa na sekta hii, madereva wanabeba uchumi utakumbuka kwenye kipindi Cha Covid 19 Madereva wameendelea kupambana kusafirisha mizigo."

Hata hivyo bw Greyson ametoa Rai kwa madereva,kutimiza wajibu wao Sambamba na waajiri wao kwa kuwa Uchumi kwa kiasi kikubwa umebebwa na sekta ya usafirishaji.

"Rai yangu kwa serikali niiombe Wizara ya kazi na ajira kuhakikisha inapitia maagizo iliyoyatoa kwa wamiliki Kama yanatekelezwa".

 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi