Dar es salaam kuanzisha Wilaya ya Kipolisi

Alhamisi , 2nd Jul , 2020

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema wanatarajia kuanzisha Wilaya mpya ya Kipolisi ya Chanika, ambapo tayari IGP Simon Sirro ameshapitisha mpango huo.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda na Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa

Akiongea katika ziara yake ndani ya jimbo la Ukonga leo Julai 2, 2020, Makonda amesema usalama ndani ya mkoa huo utakuwa ni wa uhakika zaidi kwani Wilaya hiyo ya Kipolisi itakuwa na zaidi ya askari 300.

Katika ziara hiyo Makonda aliambatana na Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa, ambapo amesisitiza kuwa wazo hilo limepitishwa na sasa Dar es salaam itakuwa sio sehemu salama kwa wahalifu.

''IGP Sirro ameshakubali na ninamshukuru mkuu wa mkoa kwa kulipigania hilo na kukubali kunipa askari kuanzia 100 hadi 300 hivyo niseme tu kuwa Uhalifu ndani ya Dar es salaam haulipi.

Zaidi sikiliza hapo chini