Jumatatu , 25th Jul , 2022

Mkoa wa Dar es salaam leo umeadhimisha siku ya kumbukizi ya mashujaa waliopigania Uhuru wa taifa kwa kufanya usafi wa mazingira na upandaji miti kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo katika viwanja vya mashujaa Mnazi Mmoja, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla, Katibu Tawala wa Mkoa huo Hassan Abbas Rugwa ambapo amesema Serikali itaendelea kuheshimu na kuthamini kazi kubwa na nzuri uliyofanywa na Mashujaa wa Taifa hili.

Hata hivyo Rugwa ameeleza kuwa kila Wilaya ndani ya mkoa huo imeadhimisha siku ya Mashujaa kwa namna yake ikiwa pamoja na kufanya usafi na upandaji wa miti, ambapo pia ameipongeza Wilaya ya Kinondoni kwa kuadhimisha siku ya Leo kwa kupanda takribani Miti 4,000.


Maadhimisho ya siku ya Mashujaa yaliyofanyika Mnazi mmoja yamehudhuriwa pia na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wastahiki Meya, Makatibu tawala, Viongozi wa Dini, Wakuu wa idara, Wadau mbalimbali