Jumatatu , 21st Nov , 2022

Zaidi ya wananchi milioni nne wa mkoa wa dar es Salaam katika halmashauri za Temeke, Kinondoni na Ilala kuanzia wenye umri wa miaka mitano wameanza kupatiwa tibakinga dhidi ya ugonjwa wa matende na mabusha kuanzia kata ya Tandale ambayo ina idadi kubwa ya wagonjwa kwa manispaa ya kinondoni

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mgaga Mkuu mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid wakati wa kuanza utekelezaji wa zoezi la utoaji wa kingatiba ya mabusha na matende kwa halimashauri ya kinondoni katika kata ya Tandale ikiwa ni mpango wa kupambana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele.

Amesema katika halmashauri zilizolengwa kupatiwa tibakinga jumla ya wananchi 4174 wana ugonjwa wa mabusha huku wenye matende wakiwa 2221.

Kwa upande wake Katibu tawala wa kinondoni ametoa wito kwa viongozi wa serikali za mitaa kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi hilo la upataji tibakinga ili kudhibit ugonjwa huo.

Tayari kampeni hiyo ya utoaji tibakinga imeanza leo 21 hadi 25 mwaka huu lengo ni kudhibiti ugonjwa huo kwani hudhohofisha nguvu kazi ya taifa.