Ijumaa , 20th Mar , 2020

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando, amemfukuza kazi mkarandasi kutoka kampuni ya LGNA CO.LTD ya Tabora, aliyekuwa anajenga barabara yenye urefu wa km 1.5, kutoka Mkokwa hadi Mnyagala Mkoani Katavi kwa kushindwa kutekeleza mradi huo.
    

Pingu

Akikagua barabara hiyo Mkuu wa wilaya amebaini kuwa, mkandarasi huyo ni kanjanja na kwamba barabara ameijenga chini ya kiwango na yuko nje ya muda.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) mkoani humo, kumshikilia mkandarasi huyo ili akaeleze namna alivyoipata kazi hiyo kwa kuwa hana vigezo.