
Mkuu wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lulimbo
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na kujibu kero za wananchi wa Kijiji cha Lulimbo wilayani humo, ambapo pia akakemea tabia ya wanaume wanaopiga wake zao na kuwataka wabadilike la sivyo watachukuliwa hatua za kisheria.
"Wanyasa ni wastaarabu bwana, hata wakiwa wanacheza Mganda wanavaa nguo nyeupe na hazichafuki hata wakicheza masaa na masaa, nguo fupi na Milege Hazitakiwi wilayani Nyasa," amesema Mkuu wa Wilaya.