Ijumaa , 10th Sep , 2021

Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Asajile Mwambambale, ili kwenda kujibu tuhuma zinazomkabili katika Halmashauri ya wilaya ya Kilosa za wizi wa mabati 1,172.

Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu

Agosti 24, 2021, Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro lilithibitisha kuwashikilia watumishi sita wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa akiwemo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo, Asajile Mwambambale, kwa tuhuma ya wizi wa mabati zaidi ya 1,172 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 31.

Aidha, taarifa hiyo iliongeza kuwa mabati hayo yalikuwa yamehifadhiwa kwenye stoo ya halmashauri hiyo na katika wizi huo hakuna kufuli wala mlango uliovunjwa.