Alhamisi , 26th Aug , 2021

Dereva teksi Daniel Ofori (37) ahukumiwa kifungo cha miezi 30 jela huko Ghana kwa kosa la kuendesha gari kwa mwendo kasi huku afisa wa Polisi akiwa kwenye boneti ya gari.

Picha ya Afisa Polisi akiwa juu ya boneti

Daniel alikuwa akifuatiliwa na Polisi tangu mwaka 2020 baada ya video ya tukio hilo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na atatumikia miaka 6 jela kwa kosa la kuendesha gari kwa mwendo kasi, miezi 24 kwa makosa ya jinai na kufungiwa leseni yake kwa kipindi cha miaka mitano.

DSP Ebenezer Tetteh, afisa Uhusiano wa Polisi wa Mkoa wa Mashariki amesema hukumu hiyo inatuma ishara nzuri kwa madereva wengine na watumiaji wa barabara.