Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Dereva wa basi lililowaka moto asakwa

Jumatatu , 9th Jul , 2018

Baada ya gari la abiria linalofanya safari zake Arusha - Dar es salaam kuteketea kwa moto  maeneo ya Tegeta,  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Marison Mwakyoma amesema bado wanamsaka dereva wa basi hilo ili kuweza kutoa maelezo ya kina juu ya ajali hiyo.

Basi lililoteketea moto siku ya jana maeneo ya Tegeta, Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na www.eatv.tv, Kamanda Mwakyoma amesema kwamba ingawa taarifa za awali zinadai kwamba ni kufeli kwa breki ya nyuma, lakini zipo sababu za msingi ambazo zinaweza kutolewa na dereva huyo kwani tukio lililopelekea gari hilo kulipuka halikuwa la ghafla.

Akizungumzia ajali hiyo iliyotokea Tegeta jana usiku, Kamanda Mwakyoma amesema kwamba basi hilo lilitokea Arusha likuwa na abiria 42, ambapo 22 walishukia Bagamoyo na wengine waliosalia walifikia maamuzi  ya kushuka
baada ya kuona gari linazidi kutoa harufu na ndipo dereva alipoamua kulitelekeza.

Aidha Mwakyoma ameongeza kwamba siyo kila ajali husababishwa na uzembe wa dereva kwani yapo mambo mengi ikiwepo nyaya za umeme kugusana, ku-jam kwa breki ya gari hivyo wamiliki wa magari wanapaswa kuwa makini wanapofanya 'service' ya magari ikiwa ni pamoja na kutazama mfumo mzima wa umeme na siyo kumwaga 'oil'.

Pamoja na hayo Mwakyoma amesema uchunguzi wa kina wa kuhusu ajali hiyo bado unaendelea kufanyika na sasa wanasubiria hati ya ukaguzi wa gari hilo kutokea Arusha kabla ya safari.

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea