
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji
Akiongea Bungeni Mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Ashantu Kijaji amesema kuwa hali hiyo inaweza kusababisha uwezekano wa kupungua thamani ya hazina ya rasimali ya nchi.
Ashantu amesema kuwa bei ya dhahabu imekuwa ikishuka kila siku kutoka dola 1745 za kimarekani, kwa wakia moja mwaka 2012 hadi dola za Marekani 1068 kufikia desemba 2015.
Aidha Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa ununuzi na uuzaji wa dhahabu unahitaji ujuzi maalum kwa kuzingatia jukumu la msingi la Benki Kuu ambayo haijajijengea uwezo katika eneo la biashara ya dhahabu.
Ameongeza kuwa hazina ya rasimali za kigeni inaweza kuwa dhahabu, fedha au fedha za kigeni na uamuzi kuhusu hazina itunzwe vipi unazingatia vigezo mbalimbali, vikiwemo kuuza dhamana ya hati fungani za serikali.