Jumanne , 19th Oct , 2021

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima, amewataka Watanzania wanaoishi na kusoma nchini Urusi kutumia fursa zilizopo Tanzania katika kuwekeza na kuwasaidia Watanzania.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima

Dkt. Gwajima ameyasema hayo jijini Saint Petersburg nchini Urusi alipokutana na kufanya mazungumzo na Watanzania wanaoishi na wanaosoma katika vyuo mbalimbali nchini humo na kusema Tanzania ina fursa nyingi za kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, utalii na madini ambazo zinaweza kuchangia katika maendeleo ya Taifa.

 "Niwaambie ndugu zangu nyumbani kumenoga, wekezeni nyumbani haijalishi wewe unaishi huku au wewe ni mwanafunzi mnaweza mkajiunga pamoja na kuanzisha umoja wenu mkatafuta wafadhili mkiwa Urusi na mkawasaidia Watanzania wenzenu," amesema Waziri Dkt. Gwajima.