Jumanne , 13th Feb , 2018

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson amefunguka kwamba bunge halikukataa  hoja binafsi ya Elimu bure pedi bure ya Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Geita, bali mchakato wa hoja hiyo ndiyo haukufikishwa ili ujadiliwe.

Dk. Tulia ameyasema hayo leo mapema wakati akiwa kwenye kipindi cha Supamix na kusema kwamba pamoja na kuwa hoja ya Mh. Peneza ilikuwa ni nzuri lakini mchakato wa kuwasilisha ndio haukukamilika.

"Sisi bungeni hoja binafsi lazima uzungumze  na wabunge wengi ili wakuunge mkono. Hoja ya Peneza ni nziuri lakini haikupitia bungeni kujadiliwa. Mchakato wa hoja hii haukuletwa bungeni halafu ukakataliwa"

Wiki iliyopita Mbunge Penneza alijaribu kupeleka hoja binafsi kuhusu wanafunzi wa kike kupatiwa pedi lakini hoja hiyo haikufanikiwa kwani hoja hiyo ilikataliwa kwa sababu yakuwa inavunja ibara ya 99 (2) ya Katiba.