
Katibu Mkuu wa CCM. Dkt. Bashiru Ali.
Akizungumza na wanachama wa CCM mkoani Dodoma leo katika mkutano wa kukusanya maoni kuhusu Muswada wa sheria ya Vyama vya siasa, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt..Bashiru Ali amesema mfumo wa vyama vingi umeiimarisha CCM.
"Sheria hii si ya kwanza kutungwa na haitakuwa sheria ya mwisho...Ukiendesha siasa kwa urasimu hutatenda haki", amesema.
Amebainisha kuwa wanatetea muswada huo kwasababu umeongeza uhakika wa utawala na kulinda misingi ya utaifa.
Aidha Dkt. Bashiru ameongeza kwamba, "Mimi natamani sana kwenye sheria hii hata koma(alama ya nukta) isiondolewe lakini mnaweza kutoa maoni yenu ya kuboresha ambayo hayaondoi maudhui", ameongeza Dkt. Bashiru.