
Kushoto ni Esther Bulaya na kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt Godwin Mollel
Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 10, 2021, Bungeni Dodoma, wakati akijibu maswali ya wabunge hao kuhusu suala la maabara ya COVID-19, tiba asili na takwimu halisi za wagonjwa na vifo vilivyotokana na ugonjwa huo.
"Ninataka nimueleweshe Mh. Mbunge kwamba toka uhuru tumekuwa na CT Scan mbili tu kwenye hospitali za mikoa, lakini amekuja tu Rais Samia tunaenda kupata CT Scan 29 ambazo zina gharama kubwa kuliko mashine za kupima corona, kazi inapigwa nyie muendelee kusherehekea, karibuni upande huu kumenoga," amesema Dkt Mollel