
Serikali mkoani Mwanza imesema kukamilika kwa jengo la mama na mtoto lililogharimu shilingi bilioni 10.1 katika hospitali ya Rufaa ya mkoa huo ya Sekoutoure kutasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto vilivyokuwa vikitokea mkoani humo.
Mkuu wa mkoa huo wa Mwanza Adam Malima amesema jengo hilo la mama na mtoto linatarajiwa kuzinduliwa mapema wiki ijayo na makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DK Phillipo Mpango atakayekuwa na ziara ya kikazi ya siku tatu, hivyo akawaomba wakazi wote kujitokeza kushuhudia uzinduzi huo
‘Makamu wa Rais ataelekea hospitali ya mkoa wa Mwanza ya Sekoutoure ambapo atazindua jengo la mama na mtoto lenye thamani ya shilingi bilioni 10.1 mradi huu utakuwa na manufaa yafuatayo utaboresha huduma ya afya kwa wananchi hususani kwa mama na watoto utapunguza msongamano kwa wagonjwa uliopo sasa ambao utatoa huduma kwa vitanda 260 palepale na tunatarajia huduma zitakazotokana na uboresha wa huduma pale sekou toure utapunguza vifo vya mama na Watoto wakati wa kujifungua na katika hatua zote za ujauzito’
Katika hatua nyingine Malima amesema Makamu wa Rais Dk Mpango atazindua chanzo cha maji kilichopo Butimba wilayani Nyamagana ambacho kinatarajiwa kuzalisha lita za maji milioni 48 kwa siku huku mahitaji yakiwa lita milioni 160 kwa siku hivyo chanzo hicho kinatarajiwa kupunguza kero ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi
‘Mradi huu mkubwa utazalisha lita milioni 48 kwa siku hili lina umuhimu mkuwa sababu jiji la Mwanza na Ilemela kwa Pamoja tuna mahitaji lita milioni 160 kwa siku mpaka sasa mamlaka za maji zinazalisha lita milioni 90 kwa siku kwahiyo tunadaiwa lita kama milini 70 kwahiyo uwekezaji unaofanywa butimba utaleta lita milioni 48 kwa wakazi wa Mwanza na mikoa ya Jirani
Katia ziara hiyo ya siku tatu makamu wa Rais pia anatarajiwa kuzindua jengo la Saratani katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya Bugando Pamoja na stendi ya mabasi ya Nyamhongolo.