Jumatano , 3rd Jun , 2020

Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, amempongeza Rais Magufuli kwa hatua aliyofikia ya ujenzi wa Ikulu ya Dodoma na kumtakia kila la heri katika safari yake hiyo na kuongeza kuwa hiyo ndiyo raha ya kujitawala kwakuwa inakupa nafasi ya kufanya vitu kwa uhuru.

Kushoto ni Rais wa Tanzania Dkt Magufuli, akiwa na Rais wa Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein.

Dkt Shein ameyabainisha hayo leo Juni 3, 2020, jijini Dodoma, wakati wa kuweka udongo katika jiwe la msingi la ujenzi huo,  mara baada ya kumaliza kikao cha ndani na mwenyeji wake Dkt Magufuli, kilichohudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt Bashiru Ally.

"Huko ndiyo kujitawala, kutawaliwa sio kuzuri na anayekutawala anafanya anavyotaka yeye kwa utashi wake pale anapotaka kufanya, tunapochukua hatua ya kujitawala wenyewe tunafanya mambo kama haya makubwa kwa ajili ya wananchi, hii ni ofisi kwa ajili ya wananchi wa Tanzania" amesema Rais Dkt Shein.